JOINT ACM ADVERT 2019

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), zinapenda kuwataarifu Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi, Makandarasi, Wahandisi na wataalam wanaoshabihiana nao kuwa mkutano wa pamoja wa mashauriano na wadau sasa utafanyika tarehe 04 hadi 05 Septemba 2019 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam badala ya tarehe 29 na 30 Agosti kama ilivyotangazwa hapo awali.