TAARIFA KWA UMMA KUAIRISHWA KWA MKUTANO-ACM 2018

Bodi ya Usajili wa Makandarasi(CRB) inasikitika  kuwatangazia Makandarasi na wadau wote wa sekta ya Ujenzi kwamba mkutano wa mashauriano wa mwaka 2018 uliokuwa ufanyike tarehe 3 hadi 4 Mei 2018 katika ukumbi wa  Dr. Jakaya Kikwete Convention  Centre, Dodoma umeahirishwa, hii kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Bodi.

Mkutano huu sasa  utafanyika tarehe 28 hadi 29 Juni 2018, katika ukumbi wa  Dr. Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma kuanzia saa 2 asubuhi.

Bodi inaomba radhi kwa usumbufu wowote  utakaojitokeza.

Kwa maelezo zaidi tafadhali usisite kuwasiliana na ofisi za Bodi za (Makao Makuu na ofisi za kanda).
 
Imetolewa na:
MSAJILI