Wednesday 8th February 2023, 23:47 pm

logo

The United Republic of Tanzania

CONTRACTORS REGISTRATION BOARD

  • crblogo

KUWASILISHA FOMU ZA MREJESHO (ARF) KWA MWAKA WA FEDHA 2021/22 KWA MTANDAO

Bodi inapenda kuwataarifu Makandarasi wote nchini kwamba muda wa kuwasilisha fomu za mrejesho (ARF) kwa mwaka wa fedha 2021/22 kwa njia ya mtandao umewadia na mwisho wa kuwasilisha ni tarehe 30 Septemba 2022. Ili kuupata mfumo wa kukuwezesha kujaza fomu ya mrejesho mtandaoni, ingiza “URL” https://cimis.crb.go.tz au fuata “link” kupitia tovuti ya Bodi, www.crb.go.tz (online services button). Watumiaji wenye akaunti walizotumia kujaza fomu hizi miaka ya nyuma au wanazotumia kusajili miradi, wazitumie akaunti hizo kuupata mfumo. Watumiaji wapya watapaswa kujisajili kuwa watumiaji wa mfumo. Kupitia mfumo wa mtandao, mtumiaji atachagua „„Register‟‟ ili kusajili akaunti yake ya kutumia mfumo. Mtumiaji atajaza taarifa zote zitakiwazo na kuchagua “Submit”. Utambulisho wa mtumiaji, “username ID” na nywila, “password” vitatumwa kwa mtumiaji kupitia barua pepe iliyoingizwa na mtumiaji kipindi cha kujisajili mtandaoni. Ili kujaza fomu ya mrejesho mtandaoni, mtumiaji wa mtandao aliyejisajili ataingia mtandaoni kupitia “URL” au “link” kwa kuingiza utambulisho wa mtumiaji, “username ID” na nywila, “password” kama ilivyoelekezwa awali. Kupitia ukurasa utakaojitokeza, mtumiaji atabofya “ARF” katika “Create new ARF”‟ na kuingiza taarifa zote zitakiwazo na kisha kubofya “Submit” baada ya kukamilisha. Mtumiaji atalazimika kurekebisha mapungufu hadi fomu itakapokubalika na mfumo. Uwasilishaji wa fomu hizi mtandaoni ni lazima ufanywe na Mkurugenzi Mkuu, “Managing Director” au Mkurugenzi wa Ufundi, “Technical Director”. Maelekezo haya ya jinsi ya kuufikia mfumo na kujaza fomu mtandaoni pia yanapatikana katika tovuti ya Bodi, www.crb.go.tz. Mwisho wa kuwasilisha fomu za mrejesho kwa mwaka wa fedha 2021/22 kwa mtandao ni tarehe 30 Septemba 2022.

Notice Board

Click "New" Icon Below To View Adverts

JV PARTNERSHIP TRAINING- JANUARY 26- 27, 2023- DODOMA
KUWASILISHA FOMU ZA MREJESHO (ARF) KWA MWAKA WA FEDHA 2021/22 KWA MTANDAO
ONLINE SUBMISSION OF ANNUAL RETURN FORMS FOR THE FINANCIAL YEAR 2021/22
CRB EVENTS CALENDAR FOR THE FINANCIAL YEAR 2022/23
ONLINE PROJECT REGISTRATION MANUAL
PROCEDURE FOR CHANGING NAMES, SHAREHOLDERS AND DIRECTORS

Video Adverts

Photo Gallery

Subscribes For Newsletter