Serikali imewaagiza Makandarasi nchini kuwa waaminifu na kufanya kazi kwa weledi uliyotukuka katika kutekeleza miradi ya umma kwa gharama halisi, kwa wakati na ubora unaotakiwa kulingana na mkataba wa kazi jambo ambalo litafanya Serikali iendelee kuwaamini.
Ni kauli ya Katibu Tawala mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana, wakati akifunga mkutano wa kwanza wa mashauriano na wadau na sekta ya ujenzi kwa mwaka 2023 uliofanyika tarehe 31/03/2023 uliyolenga kuwajengea uwezo makandarasi wa ndani.
Photo by:Admin, 2023-04-05 05:03:13 |
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Rhoben Nkori akizungumza na makandarasi waliokuwa kwenye mafunzo ya siku mbili ya kazi za ubia (JVs) yaliyoandaliwa na bodi hiyo jijini Dodoma.
Msajili wa bodi hiyo, Mhandisi Rhoben Nkori, alisema “Nawashauri wakandarasi wadogo na wakati wajitahidi kushirikiana na makandarasi wakubwa ili kwanza wapate uzoefu wa kufanyakazi kubwa badala ya kukimbilia kuomba kupanda daraja, wengine wanaghushi hadi nyaraka waonekane wamekua na vigezo vya kusajiliwa daraja la kwanza au la pili,” alisema
Alisema iwapo makandarasi watafanya miradi kwa ushirikiano wa kweli tofauti na ile ambayo wakubwa wanawasindikiza wadogo watapata uzoefu wa kazi hizo.
Photo by:Admin, 2023-02-23 06:33:41 |
Makandarasi wakifuatilia mafunzo kuhusu kufanyakazi za ubia Joint Ventures (JVs) yaliyotolewa na Bodi ya Usajili wa Makandarasi CRB mkoani Dodoma
Photo by:Admin, 2023-02-23 06:32:32 |