Saturday 27th July 2024, 13:41 pm

logo

The United Republic of Tanzania

CONTRACTORS REGISTRATION BOARD

  • crblogo

From The Press

photos are coming soon Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imesema inaanza operesheni maalum ya kukagua miradi mikubwa inayotekelezwa na Makandarasi kutoka nje ya nchi, kutokana na miradi mingi kutekelezwa chini ya viwango. Aidha imebaini hayo kufuatia ziara mbalimbali za Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa katika miradi mbalimbali ikiwemo barabara ambayo imeonekana kuwa na changamoto kubwa. Akizungumza leo jijini Arusha, katika ufunguzi wa mafunzo ya usimamizi wa fedha kwa Makandarasi,Msajili wa CRB, Rhoben Nkori, alisema Bodi hiyo imeamua kufanya operesheni hiyo maalum kuanzia mwezi Mei hadi katikati ya mwezi Juni mwaka huu. Aliwataka Makandarasi wote kutambua kuwa operesheni hiyo maalum itafanyika hadi mwezi Juni, 2024 ili kujiridhisha Makandarasi wote walioingia mkataba na serikali kama wanafanya kwa mujibu wa mikataba waliyoingia na sheria, kinyume na hapo hatua zitachukuliwa. “Bodi iemamua kufanya operesheni maalum ya kutembelea miradi na kukagua miradi yote mikubwa inayofanywa na wakandarasi wa nje kwasababu miradi mingi mikubwa inafanywa na wakandarasi wa nje,”alisema.
Photo by:Admin, 2024-05-16 06:26:32
photos are coming soon Waziri wa Ujenzi, innocent Bashungwa ameziagiza Bodi za Usajili wa Makandarasi (CRB) na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), kuhakikisha zinaandaa mpango kazi wa kusimamia na kuimarisha taaluma ya Sekta ya Ujenzi nchini ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wake ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia. Bashungwa ameyasemaa hayo leo Tarehe 06 Novemba, 2023 jijini Dodoma, alipokuwa akizindua Bodi za ushauri za CRB na ERB ambazo zinaundwa kwa mujibu wa sheria ili kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Bodi hizo. Amesema kuwa Takwimu zinaonyesha kuwa suala la upatikanaji wa fursa nchini katika utekelezaji wa miradi kwa makandarasi wa ndani haliridhishi kutokana na kuwa licha ya makandarasi wa ndani kuwa wengi bado miradi wanayoitekeleza ni michache ukilinganisha na makandarasi wa nje. “Muandae mpango kazi wa kusaidia Makandarasi wa ndani, muujadili, kuutathmini na kuusimamia kwa pamoja badala ya kulalamika makandarasi wa ndani hawapati fursa”, amesema Bashungwa. Pia, Bashungwa amesisitiza kwa bodi hizo kuongeza ushirikiano mzuri walionao ili kusaidia taaluma hiyo kufanya kazi vizuri na kuleta maendeleo nchini.
Photo by:Admin, 2023-11-07 06:02:40
photos are coming soon Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ameagiza Wizara kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), kuhakikisha wanakuja na mikakati ya kuwawezesha Makandarasi Wazawa kushirki katika Utekelezaji wa miradi ya Sekta ya Ujenzi nchini ili kuleta tija kwa Makandarasi hao na Taifa kwa ujumla. Ameyasema hayo Septemba 26, 2023 jijini Dodoma, wakati alipokutana na kupokea taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Taasisi za Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC). Bashungwa ameagiza Wizara kukaa na kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kuandaa mikakati itakayosaidia makandarasi hao kutekeleza miradi mingi hasa ya kimkakati itakayoweza kuinua mitaji yao. “Linapokuja suala la ‘Local content’ yaani fursa za kiuchumi kwa watanzania, Mheshimiwa Rais kiu yake ni kuona ushiriki wa Makandarasi wazawa kwenye maendeleo ya Sekta ya Ujenzi unaongezeka”, amesema Bashungwa. Bashungwa ameeleza kuwa Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa idadi ya Makandarasi waliosajiliwa na Bodi ni 14,550 ambapo kati ya hao 550 ni Makandarasi wa nje na 14,000 ni Makandarasi wazawa lakini katika utekelezaji wa miradi Makandarasi Wazawa wanapata asilimia 46 na Makandarasi wa nje wanapata asilimia 54. Aidha, Bashungwa ameishukuru Serikali kupitia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maboresho aliyoayaagiza katika sheria ya manunuzi kwa miradi yenye gharama ya kutoka Bilioni 10 hadi 50 kupewa kipaumbele kutekelezwa na makandarasi wazawa ili kuwajengea uwezo. Kuhusu madeni kwa Makandarasi, Waziri Bashungwa amesema kuwa kupitia Wizara ya Fedha, Serikali imeshaweka utaratibu wa kulipa madeni hayo ambapo hivi sasa kila mwezi kuanzia mwezi wa nane kiasi cha Bilioni 70 kinatengwa ambapo Bilioni 50 zinalipa madeni ya makandarasi wa ndani na Bilioni 20 ni kwa ajili ya kulipa Makandarasi wa nje. Bashungwa pia ameziagiza Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi kuhakikisha zinabuni mikakati ya kutangaza mafanikio na kazi zao kwa umma ili kuleta tija katika Taasisi hizo na Taifa kwa ujumla. Kadhalika, Bashungwa ameziagiza Taasisi hizo kusimamia wataalamu wao ili kuhakikisha wanatoa huduma sahihi na kwa wakati kwa umma na kuhakikisha wanachukua hatua kwa wale ambao watakiuka maadili ya kazi zao.
Photo by:Admin, 2023-09-27 08:34:12

Notice Board

Click "New" Icon Below To View Adverts

LIST OF FOREIGN CONTRACTORS WITH OUTSTANDING ANNUAL FEES INTENDED FOR DELETION
LIST OF LOCAL CONTRACTORS WITH OUTSTANDING ANNUAL FEES INTENDED FOR DELETION
DELETION OF CONTRACTORS
CONTRACTORS REVIEW INFORMATION FORM
ONLINE PROJECT REGISTRATION MANUAL
PROCEDURE FOR CHANGING NAMES, SHAREHOLDERS AND DIRECTORS

Video Adverts

Photo Gallery

Subscribes For Newsletter