Saturday 27th April 2024, 09:36 am

logo

The United Republic of Tanzania

CONTRACTORS REGISTRATION BOARD

  • crblogo

From The Press

photos are coming soon MAKANDARASI nchini wameelezwa kuwa matumizi ya mfumo wa manunuzi ya umma kielekroniki (TANePS) ni ya lazima kwao hivyo wanapaswa kuufahamu vyema na kuutumia kwaajili ya kuwasilisha zabuni zao mapema. Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB),Qs Joseph Tango, wakati wa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huo na wajibu wa mkandarasi. Tango alisema ni muhimu kwa makandarasi kufanya maandalizi ya zabuni mapema na kuziwasilisha kwa njia ya mfumo huo kama ni mradi wa serikali kwani tabia ya kufanya kwa mtindo wa zimamoto hauwezi kuleta matokeo mazuri. “Kwenu nyinyi ujuzi wa kutumia mfumo huu wa kielektroniki ni lazima kwasababu mwajiri mkubwa wa mkandarasi ni serikali na kwa sasa huwezi kushiriki zabuni ya kazi za serikali bila kupitia mfumo huu.” alisema “Na mjenge kawaida ya kufanya mapema kwani mfumo huu ni wa kielektroniki na chochote kinaweza kutokea na kukufanya uchelewe kuwasilisha zabuni kwa mfano hitilafu ya umeme mahali ulipo au udhaifu wa mtandao wa intaneti haya yote yatakukwamisha.” Alisema. Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Qs. Joseph Tango akifunga mafunzo ya siku tatu kuhusu wajibu wa makandarasi na namna ya kujaza zabuni kielektroniki yaliyoendeshwa na bodi hiyo mkoani Morogoro kwa siku tatu na kumalizika siku ya Ijumaa. SOURCE: "HABARILEO JUMATATU AGOSTI 16,2021","Nipashe Jumatatu Agosti 16,2021"
Photo by:Admin, 2021-08-17 11:39:52

Notice Board

Click "New" Icon Below To View Adverts

Video Adverts

Photo Gallery

Subscribes For Newsletter